• HABARI MPYA

  Sunday, April 21, 2019

  HIMID MAO AISAIDIA PETROJET KUIPIGA NOGOOM 2-1 KATIKA MCHEZO WA LIGI YA MISRI

  Na Mwandishi Wetu, SUEZ
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami jana amecheza kwa dakika zote 90, timu yake  Petrojet FC ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Nogoom katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri Uwanja wa Jeshi la Misri mjini Suez.
  Nogoom walitangulia kwa bao la dakika ya 45 na ushei la Salah Amin kabla ya Ahmed Afifi kufunga mawili dakika ya 66 na 90 kuitoa nyuma Petrojet kuibuka na ushindi huo.
  Kwa ushindi huo, Petrojet inafikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 30 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Misri inayoshirikisha timu 18.

  Hali inazidi kuwa mbaya kwa Nogoom ambayo inaendelea kuburuza mkia ikibaki na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 29.
  Vigogo Zamalek ndiyo wanaongoza ligi hiyo kwa pointi zao 60 za mechi 26, wakifuatiwa Pyramids yenye pointi 60 pia za mechi 28, wakati Al Ahly ni ya tatu kwa pointi zake 58 za mechi 26.
  Kikosi cha Nogoom kilikuwa; Ahmed Abdel Fattah, Mahmoud Fathalla, Khaled Abdelrazek, Ahmed Ayman, Karim Fouad/Girgis Saleh dk90+1, Didier Kore, Islam El Far/ Ayman El Ghobashy dk59, Amr El Sisi, Salah Amin, Tosin Omoyele na Mohab Yasser/ Joel Lamah dk75.
  Petrojet; Mohamed Abou Elnaga, Islam Siam/Chris Gadi dk80, Hossam Hassan, Hamada Galal, Ahmed Salem Safi, Mahmoud Salah/Mohamed Sanogo Vieira dk59, Himid Mao, Ahmed Afifi/ Ahmed El Agouz dk90+2 , Mahmoud Emad, Ahmed Abdel Rahman ‘Zola’ na Shokry Naguib.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HIMID MAO AISAIDIA PETROJET KUIPIGA NOGOOM 2-1 KATIKA MCHEZO WA LIGI YA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top