• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 15, 2019

  CAMEROON YAIPIGA GUINEA 2-0, MOROCCO NA SENEGAL SARE 1-1

  CAMEROON imeanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Guinea katika mchezo wa Kundi B jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Steve Regis Mvoue alifunga bao la kwanza dakika ya 42 akimalizia pasi ya kiungo mwenzake,  Saidou Alioum Moubarak, kabla ya kumsetia mshambuliaji Leonel Wamba Djouffo kufunga la pili dakika ya 72.
  Mchezo mwingine wa Kundi B leo, Morocco imetoa sare ya 1-1 na Senegal hapo hapo Uwanja wa Azam Complex, unaomilikiwa na klabu ya Azam FC. 

  Wachezaji wa Cameroon wakishangilia shindi wa mabao 2-0 dhidi ya Guinea leo Uwanja wa Azam Complex 

  Mshambuliaji Tawfik Bentayeb alianza kuifungia Morocco dakika ya 47 akimalizia pasi ya kiungo Faissal Boujemaoui, kabla ya mshambuliaji Aliou Badara Balde kuisawazishia Senegal dakika ya 88 akimalizia kazi nzuri ya kiungo Samba Diallo.
  Ikumbukwe mechi za ufunguzi jana, wenyeji Tanzania walianza vibaya baada ya kuchapwa mabao 5-4 na Nigeria huku jirani zao, Uganda nao wakipigwa 1-0 na Angola.
  Kesho ni mapumziko na michuano hiyo itaendelea kesho, Nigeria wakianza kumenyana na Angola Saa 10:00 jioni kabla ya Serengeti Boys kumenyana na jirani zao, Uganda Saa 1:00 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAMEROON YAIPIGA GUINEA 2-0, MOROCCO NA SENEGAL SARE 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top