• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 16, 2019

  MECHI ZA MTIBWA SUGAR NA YANGA, COASTAL NA SIMBA KUANZA SAA 8:00 MCHANA KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MECHI zote za Ligi Kuu ya Tanzania Bara kesho zitaanza Saa 8:00 mchana badala ya Saa 10:00 jioni kama ilivyopangwa awali.
  Mtibwa Sugar watawakaribisha Yanga SC Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na Coastal Union watakuwa wenyeji wa Simba SC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
  Bodi ya Ligi imeamua mechi hizo zifanyike mchana badala ya jioni ili kutoa fursa kwa Watanzania kufuatilia michuano Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) zinazoendelea mjini Dar es Salaam. 

  Leo ni mapumziko na michuano hiyo itaendelea kesho, Nigeria wakianza kumenyana na Angola Saa 10:00 jioni kabla ya Tanzania kumenyana na jirani zao, Uganda Saa 1:00 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Na hiyo ni baada ya jana Cameroon kushinda 2-0 dhidi ya Guinea na Morocco ikitoa sare ya 1-1 na Senegal Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam katika mechi za Kundi B. 
  Ikumbukwe mechi za ufunguzi juzi, wenyeji Tanzania walianza vibaya baada ya kuchapwa mabao 5-4 na Nigeria huku jirani zao, Uganda nao wakipigwa 1-0 na Angola.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MECHI ZA MTIBWA SUGAR NA YANGA, COASTAL NA SIMBA KUANZA SAA 8:00 MCHANA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top