• HABARI MPYA

  Thursday, April 18, 2019

  AZAM FC YAANGUKA NANGWANDA SIJAONA, YACHAPWA 1-0 NA NDANDA FC MTWARA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imeteleza baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara jioni ya leo.
  Shujaa wa Ndanda FC jioni ya leo ni nyota wake, Mohammed Mkopi aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 62 akitumia udhaifu wa mabeki wa Azam FC.
  Na kwa ushindi huo, Ndanda FC inafikisha pointi 43 baada ya kucheza mechi 32 na kujiinua kutoka nafasi ya 11 hadi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

  Azam FC yenyewe inabaki na pointi zake 66 baada ya kucheza mechi 32, ikiendelea kukamata nafasi ya pili, nyuma ya vinara, Yanga SC wenye pointi 74 za mechi 2 na mbele ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 60 za mechi 23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAANGUKA NANGWANDA SIJAONA, YACHAPWA 1-0 NA NDANDA FC MTWARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top