• HABARI MPYA

  Sunday, April 21, 2019

  BARCELONA YAENDELEA KUNG'ARA, YAIPIGA 2-1 REAL SOCIEDAD LA LIGA

  Jordi Alba akishangilia na mchezaji mwenzake, Arturo Vidal baada ya kuifungia Barcelona bao la pili dakika ya 64 akimalizia pasi ya Lionel Messi ikiilaza 2-1 Real Sociedad katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Camp Nou. Bao la kwanza lilifungwa na Clément Lenglet dakika ya 45 akimalizia pasi ya Ousmane Dembele kabla ya Juanmi kuisawazishia Real Sociedad dakika ya 62 kwa pasi ya  Mikel Merino na kwa ushindi huo, Barcelona inafikisha pointi 77 baada ya kucheza mechi 33 ikiendelea kuongoza La Liga kwa pointi tisa zaidi ya Atlético Madrid 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCELONA YAENDELEA KUNG'ARA, YAIPIGA 2-1 REAL SOCIEDAD LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top