• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 18, 2019

  NI LIVERPOOL NA BARCA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA

  Wachezaji wa Liverpool wakishangilia ushindi wao wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Porto FC jana kwenye mchezo wa marudiano Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja waDo Dragao mjini Porto, Ureno hivyo kutinga Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 6-1 kufuatia kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza England wiki iliyopita na sasa itamenyana na Barcelona iliyoitoa Manchester United. Mabao ya Liverpool jana yalifungwa na Sadio Mane dakika ya 26, Mohamed Salah dakika ya 65, Roberto Firmino dakika ya 77 na Virgil van Dijk dakika ya 84, wakati la Porto lilifungwa na Eder Militao dakika ya 68 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI LIVERPOOL NA BARCA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top