• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 24, 2019

  FAINALI AFCON U17 DAR 2019 NI CAMEROON NA GUNEA, NIGERIA YADODA

  TIMU za Cameroon na Guinea zitakutana katika Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON) Jumapili Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Hiyo ni baada ya zote kushinda mechi zao za Nusu Fainali kwa mikwaju ya penalti kufuatia kumaliza dakika 120 bila kufungana na wapinzani wao.
  Ilianza Guinea kuitoa Nigeria kwa penalti 10-9 kabla ya Cameroon kuitoa Angola kwa penalti 4-3, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Taifa.

  Sasa Nigeria itamenyana na Angola katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu Jumamosi Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa.
  Ikumbukwe, zote Cameroon na Guinea zilikuwa Kundi B pamoja na Senegal na Morocco, wakati Nigeria na Angola zilikuwa Kundi A pamoja na wenyeji, Tanzania na jirani zao, Uganda. 
  Pamoja na kutolewa, Nigeria na Angola zitaungana na Cameroon na Guinea kucheza Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil baadaye mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FAINALI AFCON U17 DAR 2019 NI CAMEROON NA GUNEA, NIGERIA YADODA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top