• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 21, 2019

  CRYSTAL PALACE YAIGONGA ARSENAL 3-2 PALE PALE EMIRATES

  Wilfried Zaha akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia Crystal Palace bao la pili dakika ya 61 katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates. Mabao mengine ya Palace yamefungwa na Christian Benteke dakika ya 17 na James McArthur dakika ya 69, wakati ya Arsenal yamefungwa na Mesut Ozil dakika ya 47 na Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 77.
  Kwa matokeo hayo, Crystal Palace inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 35 katika nafasi ya 12 na Arsenal inabaki nafasi ya nne na pointi zake 66 za mechi 34 pia sawa na Chelsea iliyo nafasi ya tano kwa kuzidiwa wastani wa mabao 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CRYSTAL PALACE YAIGONGA ARSENAL 3-2 PALE PALE EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top