• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 19, 2019

  PEDRO APIGA MBILI CHELSEA YASHINDA 4-3 KUTINGA NUSU FAINALI

  Pedro akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Chelsea dakika ya tano na 27 ikiibuka na ushindi wa 4-3 dhidi ya Slavia Prague katika mchezo wa marudiano Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Stamford Bridge mjini London. Mabao mengine ya Chelsea yalifungwa na Simon Deli aliyejifunga dakika ya tisa na Olivier Giroud dakika ya 17, wakati ya Slavia Prague yalifungwa na Tomas Soucek dakika ya 25 na Petr Sevcik dakika za 51 na 54 na kwa matokeo hayo The Blues inakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-3 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Praha na sasa itamenyana na Eintracht Frankfurt 
    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PEDRO APIGA MBILI CHELSEA YASHINDA 4-3 KUTINGA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top