• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 25, 2019

  ARSENAL 'YATEPESHWA', YATANDIKWA 3-1 NA WOLVERHAMPTON

  Kiungo Mjerumani, Mesut Ozil na wachezaji wenzake wa Arsenal wakisikitika baada ya timu yao kuchapwa mabao 3-1 na Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Molineux, West Midlands. Mabao ya Wolves yamefungwa na Ruben Neves dakika ya 28, Matt Doherty dakika ya 37 na Diogo Jota dakika ya 45 na ushei, wakati la Arsenal limefungwa na Sokratis Papastathopoulos dakika ya 80.
  Arsenal inaondolewa tena 'Top Four' ikishukia nafasi ya tano  baada ya kipigo cha leo ikibaki na pointi zake 66 baada ya kucheza mechi 35, ikizidiwa pointi moja na Chelsea inayoshika nafasi ya nne kwa sasa, wakati Wolves imefikisha pointi 51 katika mchezo wa 35 pia na kupanda kwa nafasi tatu hadi ya saba 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL 'YATEPESHWA', YATANDIKWA 3-1 NA WOLVERHAMPTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top