• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 28, 2017

  ZIDANE AWAWEKA MKAO WA KULA MAN UNITED KWA BALE

  KOCHA Mfaransa, Zinedine Zidane ameiweka mkao wa kula Manchester United ya England kwa kusema anaweza asiwe tayari kumbakiza winga Gareth Bale katika klabu yake, Real Madrid ya Hispania.
  Mustakabali wa Bale Uwanja wa Bernabeu upo shakani kwa mara nyingine tena, huku mabingwa hao wa Ulaya wakijaribu kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji kinda, Kylian Mbappe kutoka Monaco ya Ufaransa kwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 160.
  Inafahamika kwamba, kocha wa Real anaweza ‘kujitoa muhanga’ kwa kumuachia mmojawapo kati ya Cristiano Ronaldo, Karim Benzema au Bale ili kupata nafasi ya kumsajili Mbappe — na mchezaji huyo wa Wales ndiye aliye hatarini kuondoka.
  Mustakabali wa Gareth Bale upo Real Madrid baada ya klabu hiyo kuingia kwenye mpango wa kumsajili Kylian Mbappe kutoka Monaco ykwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 160 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Zidane aliulizwa kuhusu hilo baada ya kipigo cha Madrid cha mabao 4-1 kutoka Manchester City mjini Los Angeles mapema Alhamisi na akajibu: “Natumai BBC (Bale, Benzema na Cristiano) watabaki kwa msimu huu. Nafikiri kila mmoja anabaki. Nataka kila mmoja aliye hapa abaki, lakini chochote kinaweza kutokea hadi Agosti 31,”.
  Jose Mourinho hajafanya siri katika nia yake ya kusajili mchezaji mpya wa pembeni dirisha hili na amemlenga winga wa Inter Milan, Ivan Perisic anayeuzwa kwa Pauni Milioni 48.
  Mourinho aliibua tetesi hizo wakati United inacheza na Real mjini Santa Clara wikiendi iliyopita na alisikika akisema: “Siwezi kununua kwa sababu huzungumzi na mimi!’
  Bale, mwenye umri wa miaka 28, alisema baada ya mchezo huo kwamba ana furaha Madrid, lakini kuwasili kwa Mbappe kunaweza kuilazimisha klabu kumuuza yeye. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZIDANE AWAWEKA MKAO WA KULA MAN UNITED KWA BALE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top