• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 26, 2017

  MANE, INGS WAREJEA KIKOSINI LIVERPOOL WAKIWA KAMILI

  NYOTA Sadio Mane na Danny Ings jana wamerejea kwenye mazoezi ya Liverpool viwanja vya Melwood baada ya kupona maumivu 
  Baada ya kuwa Hong Kong kuwania taji la Ligi Kuu Asia, Wekundu hao wamerudi kwa muda Uingereza kabla ya kusafiri tena kwenda Ujerumani kwa maandalizi ya msimu mpya.
  Na kocha Jurgen Klopp anafanya jitihada kubwa kukiweka sawa kikosi chake kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

  Nyota Sadio Mane akiruka kihunzi kwenye mazoezi ya Liverpool baada ya kurejea kwenye programu kamili ya timu kufuatia kupona maumivu ya goti PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Kocha huyo wa Liverpool atazipokea kwa furaha habari za kurejea kwa Mane na Ings, ambao wamekuwa nje tangu mwezi Aprili kwa maumivu ya goti.
  Alipata pia nafasi ya kumuona Robertson anavyofiti kwenye timu yake baada ya kusajiliwa kwa Pauni Milioni 8 kutoka Hull City.
  Winga kutoka Roma, Mohamed Salah, mshambuliaji kutoka Chelsea, Dominic Solanke na beki wa kushoto, Andrew Robertson ndiyo wachezaji pekee wapy waliowasili Anfield dirisha hili.
  Liverpool inatarajiwa kusafiri kwenda Ujerumani leo kwa maandalizi zaidi ya msimu mpya, ambako itacheza michezo ya kujipima nguvu na Hertha Berlin, Bayern Munich na ama Atletico Madrid au Napoli.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANE, INGS WAREJEA KIKOSINI LIVERPOOL WAKIWA KAMILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top