• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 26, 2017

  ABDI BANDA AJIHAKIKISHIA NAMBA ‘SAUZI’ MAPEMAAA

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Hassan Banda amefanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha Baroka FC ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini mapema tu baada ya kusajiliwa kutoka Simba ya nyumbani, Tanzania.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo kwa simu kutoka Afrika Kusini, Banda amesema kwamba tangu amejiunga na timu hiyo wiki mbili zilizopita wamekwishacheza mechi tatu za kujipima nguvu na zote amecheza, tena kwa dakika zote 90.
  Amesema mechi hizo, ya kwanza walishinda na timu ya Daraja la Kwanza wakashinda 8-0, ya pili jana wakatoa sare ya 1-1 Real Eagles kabla ya leo kushinda 5-1 dhidi ya Amazulu.
  Abdi Banda amefanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha Baroka FC ya Afrika Kusini 

  “Ninamshukuru Mungu ninaendelea vizuri hapa, jana tulicheza mchezo wa kirafiki na Real Eagles tukatoa sare ya 1-1 na leo tumecheza na Amazulu tumewafunga 5-1 na mechi zote nimepangwa na kucheza dakika zote 90,”amesema.  
  Banda amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Baroka ya Ligi Kuu mapema mwezi huu baada ya kung’ara katika michuano ya Kombe la COSAFA Castle nchini Afrika Kusini akiiwezesha Tanzania kushika nafasi ya tatu.
  Banda alikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichocheza michuano ya COSAFA Castle na kutwaa Medali ya Shaba baada ya ushindi wa penalti 4-2 Julai 7, mwaka huu dhidi ya Lesotho kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 usiku wa jana Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, tena akipiga moja ya matuta hayo manne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ABDI BANDA AJIHAKIKISHIA NAMBA ‘SAUZI’ MAPEMAAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top