• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 29, 2017

  'CHAMPION BOY' MBWANA SAMATTA KAZINI UBELGIJI LEO

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta 'Champion Boy' leo anatarajiwa kuiongoza klabu yake, KRC Genk katika mchezo wa kwanza wa msimu wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.
  Nahodha huyo wa Taifa Stars anaingia kwenye msimu mpya wa ligi hiyo, baada ya maandalizi mazuri, ikiwemo kucheza mechi ya kujipima dhidi ya Everton ya England.
  Samatta na Genk wanatarajiwa kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya Ubelgiji leo kwa kuwakaribisha Waasland-Beveren Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk kuanzia Saa 3:00 usiku.
  Mbwana Samatta 'Champion Boy' leo anatarajiwa kuiongoza KRC Genk katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Ubelgiji

  Kabla ya kucheza na Everton Uwanja wa Luminus Arena na kutoa sare ya 1-1, Samatta akiisawazishia Genk baada ya Wayne Rooney kuanza kuifungia Everton, timu hiyo ilikwenda Uholanzi na kucheza mechi tatu za kujipima nguvu, ikiwemo dhidi ya Ajax iliyoisha kwa sare ya 3-3. Tangu Januari mwaka jana alipojiunga na Genk akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Samatta amecheza jumla ya mechi 55 za mashindano, 34 akianza na 21 akitokea benchi.
  Katika mechi hizo, mshambuliaji huyo wa zamani wa African Lyon, zamani Mbagala Market na Simba zote za Dar e Salaam, amefunga jumla ya mabao 18 huku akionyeshwa kadi za njano mara nne na hajawahi kutolewa kwa kadi nyekundu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: 'CHAMPION BOY' MBWANA SAMATTA KAZINI UBELGIJI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top