• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 30, 2017

  PRISONS MABINGWA KOMBE LA HISANI MBEYA, WAIPIGA YANGA B 3-1

  Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania, Godfrey Simbeye, akimkabidhi Kombe, Nahodha wa timu ya Tanzania Prisons, Laurian Mpalile, baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga U20 katika mchezo wa Hisani wa fainali wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Dk. Leonard Maboko (kulia kwake) ni Katibu wa TFF Mkoa wa Mbeya, (kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda.
  Kiungo wa Yanga B, Said Mussa (kushoto) akiudhibiti mpira mbele ya mchezaji wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid kwenye mchezo huo  
  Beki wa Tanzania Prisons, James Mwasote akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga B, Samuel Greyson 
  Mshambuliaji wa Yanga B, Festo Geryson (kushoto) akiwania mpira wa juu na beki wa Tanzania Prisons, James Mwasote 
  Wachezaji wa Prisons katika picha ya pamoja na Medali zao jana Uwanja wa Sokoine 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PRISONS MABINGWA KOMBE LA HISANI MBEYA, WAIPIGA YANGA B 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top