• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 26, 2017

  CAF YASOGEZA MBELE MTOANO MECHI ZA KLABU AFRIKA

  KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imesogeza mbele mechi za hatua ya mtoano ya michuano ya klabu barani Afrika.
  Maamuzi hayo yamefanyika katika kikao cha Kamati ya Utendaji Alhamisi iliyopita Julai 20, mwaka huu na yanahusu michuano ya Kombe la Shirikisho na Ligi y Mabingwa Afrika.
  Mechi za kwanza za Robo Fainali za mashindano hayo yote mawili zitachezwa wikiendi ya Septemba 15 naa 17 na marudiano yatakuwa wikiendi ya Septemba  22 na 24 mwaka huu, 2017.
  Awali Robo Fainali ilikuwa zifanyike Septemba 8 na 10, mwaka huu na marudiano yawe Septemba 15 na 17, wakati mechi za kwanza za Nusu Fainali hazijabadilishwa, zitachezwa kama kawaida wikiendi ya Septemba 29 na Oktoba 1, 2017.
  Lakini mechi za marudiano za Nusu Fainali zenyewe zimesogezwa mbele hadi Oktoba 20 na 22 kutoka Oktoba 13 na 15,  2017.
  Wakati huo huo, Fainali za mashindano yote mawili zinabaki kama zilivyopangwa tangu awali.

  RATIBA KAMILI MECHI ZA MTOANO AFRIKA:
  Robo Fainali: Septemba 15-17, 2017 (mechi za kwanza)
                        Septemba 22-24,  2017 (mechi za marudiano)
  Nusu Fainali: Septemba 29 Oktoba 1, 2017 (mechi za kwanza)
          Oktoba 20-22, 2017 (mechi za marudiano)
  Ligi ya Mabingwa Fainali: Oktoba 27-29 (Mechi ya kwanza)
                Novemba 3-5, 2017 (Mechi ya marudiano)
  Kombe la Shirikisho Fainali: Novemba 17-19 2017 (Mechi ya kwanza)
                Novemba 24-26, 2017 (Mechi ya marudiano)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAF YASOGEZA MBELE MTOANO MECHI ZA KLABU AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top