CHELSEA YAFIKISHA 20 WA KUTOA KWA MKOPO, BADO KAMA 15 HIVI
IDADI ya wachezaji wa Chelsea waliotolewa kwa mkopo imefika 20 baada ya mabeki, Tomas Kalas na Michael Hector kujiunga na timu za Fulham na Hull City za Ligi Daraja la Kwanza, maarufu kama Championship.
Kalas atacheza kwa msimu wa pili kwa mkopo Fulham baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka minne Chelsea, wakati Hector atafanya kazi chini ya kocha wa Chui, Mrusi Leonid Slutsky, rafiki wa Roman Abramovich Uwanja wa KCOM.
Biashara ya mkopo haitarajiwi kuwa imefikia kikomo Chelsea na wachezai 15 zaidi wanatarajiwa kutolewa kwa mkopo kabla ya dirisha hili la usajili kufungwa.
Michael Hector amekuwa mchezaji wa 20 kutolewa kwa mkopo Chelsea, baada ya leo kujiunga na Hull City PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Ogun donates land to FG to develop inland dry port
-
From Idu Jude, Abuja The Government of Ogun State has donated over 130
hectares of land to the federal government of Nigeria for the development
of an in...
0 comments:
Post a Comment