• HABARI MPYA

  Monday, July 31, 2017

  AISHI MANULA AINGIA KAMBINI SIMBA, SASA BADO NIYONZIMA TU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Simba umesema kipa wa kimataifa wa Tanzania, Aishi Salum Manula kesho ataanza mazoezi nchini Afrika Kusini baada ya kujiunga na kambi ya timu hiyo iliyopo eneo la Eden Vale mjini Johannesburg kwa maandalizi ya msimu mpya.
  Mkuu wa Idara y Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Sunday Manara amesema leo kwamba 
  Manula ambaye ndiye kipa namba moja kwa sasa nchini atakwenda kambini kesho Afrika Kusini baada ya kukamilisha taratibu zote za kujiunga na Wekundu hao wa Msimbazi, kutoka Azam FC, zote za Dar es Salaam.
  Aishi Manula kesho anatarajiwa kuanza mzozezi na timu yake mpya, Simba katika kaambi ya Afrika Kusini kujiandaa na mimu mpya

  Baada ya Aishi kuingia kambini Simba, mchezaji ambaye amebaki anasubiriwa kukamilisha orodha ya wachezaji wanaotarajiwa kuwamo katika kikosi cha Simba msimu ujao, ni kiungo Mnyarwanda,  Haruna Hakizimana Fadhili kutoka kwa mahasimu, Yanga ambako amedumu kwa miaka sita
  Wakati huo huo kesho timu ya Simba inatarajiwa kucheza mechi ya kwanza ya maandalizi ya msimu dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika Orlando Pirates ya nchini Afrika kusini. 
  Orlando ambayo ndio klabu maarufu zaid nchini humo, imeahidi kushusha silaha zake zote muhimu ili kuwapa maandalizi ya kutosha Simba, mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye dimba la Orlando liliopo jijini Johannesburg. 
  Mechi nyingine ya mwisho itakayochezwa na Simba nchini humo itapigwa siku ya Alhamis ya wiki hii dhidi ya mabingwa wa soka nchini humo kwa sasa Bidvest.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AISHI MANULA AINGIA KAMBINI SIMBA, SASA BADO NIYONZIMA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top