• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 24, 2017

  ZAMBIA NAYO YASONGA MBELE CHAN, KUMENYANA NA BAFANA

  ZAMBIA ni miongoni mwa timu zilizofuzu hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) nchini Kenya mwaka 2018 baada ya ushindi wa mabao 3-0 nyumbani dhidi ya Swaziland.
  Ushindi huo katika amchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Mashujaa mjini Lusaka, unaifanya Chipolopolo isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-0 , kufuatia awali kushsinda 4-0 kwenye mchezo wa kwanza mjini Lobamba.
  Mabao ya Justin Shonga na Brian Mwila pamoja na moja la beki Simon Silwimba yalitosha kuipeleka mbele Zambia.
  Shonga alianza kufunga dakika ya pili akimtungua kipa Sandile Ginindza, kabla ya Mwila kufunga la pili dakika ya 41 na Silwimba kumalizia dakika ya 45.
  Aidha, ushindi huo unakuwa wa kwanza nyumbani kwa kocha Wedson Nyirenda tangu aanze kazi Septemba mwaka jana baada ya awali kufungwa 2-1 na Nigeria mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2018 na 1-0 dhidi ya Msumbiji mechi ya kufuzu AFCON ya Cameroon 2019.
  Wakati huo huo, Zambia itamenyana na Bafana Bafana ambayo iliifunga Botswana 1-0 Jumamosi pia mjini Moruleng na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-0.
  Mshindi wa jumla baada ya mechi zote atafuzu moja kwa moja Fainali za CHAN mwakani nchini Kenya.

  MATOKEO KWA UJUMLA MECHI ZA KUFUZU CHAN
  Kanda ya Mashariki na Kati
  Julai 22, 2017:  Kampala Uganda 5-1 South Sudan (0-0)
  Julai 22, 2017:  Kigali Rwanda 0-0 Tanzania (1-1)
  Julai 23, 2017:  Bujumbura  Burundi vs Sudan*
  Kanda ya Magharibi A
  Julai 22, 2017:  Dakar Senegal 3-1 Sierra Leone (1-1)
  Julai 22, 2017:  Bamako Mali 4-0 Guinea (0-0)
  Julai 22, 2017:  Conakry  Guinea 7-0 Guinea Bissau (3-1)
  Julai 23, 2017:  Nouakchott Mauritania vs Liberia (2-0)
  Kanda ya Magharibi B
  Julai 23, 2017:  Cotonou Benin vs Togo (1-1)
  Kanda ya Kusini
  Julai 22, 2017:  Moruleng  Afrika Kudini 1-0 Botswana (2-0)
  Julai 22, 2017:  Lusaka Zambia 3-0 Swaziland (4-0)
  Julai 23, 2017:  Maseru Lesotho vs Comoros (0-2)
  Julai 23, 2017:  Maputo   Msumbiji vs Madagascar (2-2)
  Julai 23, 2017:  Luanda Angola vs Mauritius (1-0)
  Julai 23, 2017   Harare Zimbabwe vs Namibia (0-1)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZAMBIA NAYO YASONGA MBELE CHAN, KUMENYANA NA BAFANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top