• HABARI MPYA

    Monday, July 31, 2017

    MATOKEO YA MWISHO USAILI TAFCA, KAMPENI ZAANZA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Soka Tanzania (TAFCA), Ramadhani Mambosasa ametangaza orodha ya majina sita ya mwisho ya wagombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.
    Kwa mujibu Mambosasa, wagombea hao kwa sasa hawana budi kuendelea na kampeni hadi Agosti 9, mwaka huu ambako uchaguzi huo umepangwa kufanyika kufanyika Agosti 10, mwaka huu mjini Dodoma.
    Waliopitishwa katika orodha ya mwisho kuwania nafasi mbalimbali za uongozi - ngazi ya taifa ni pamoja na Kidao Wilfred, Lister Manyara, Michael Bundala, Dismas Haonga, Jamhuri Kihwelo, George Komba, Samuel Moja na Maka Mwalwasi na Mohammed Tajdin.
    Freddy Felix Minziro mmoja wa makocha maarufu Tanzania
    Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MATOKEO YA MWISHO USAILI TAFCA, KAMPENI ZAANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top