• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 28, 2017

  NEYMAR AGOMBANA MAZOEZINI BARCA, AKASIRIKA ASUSA NA KUTOKOMEA

  Neymar leo amegombana na mchezaji mwenzake, Semedo mazoezini kabla ya kususa na kuondoka mazoeizni PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  MJUE SEMEDO MCHEZAJI MPYA WA BARCELONA?

  Semedo mwenye umri wa miaka 23 ni beki wa kulia aliyejiunga na Barcelona dirisha hili la usajili kutoka Benfica.
  Ameigharimu timu Pauni Milioni 27 na ndiye mchezaji pekee wa maana aliyesajiliwa Barca dirisha hili hadi sasa.
  Semedo amesema amejiunga na Barca baada ya kuwa akimpenda sana mshindi wa zamani wa Ballon d'Or aliyecheza kwa vigogo hao wa Kaqtalunya, Ronaldinho Gaucho. 
  MSHAMBULIAJI Mbrazil, Neymaejiondoa kwenye mazoezini ya Barcelona na kuongeza uwezekano wa kuondoka kwa vigogo wa Hispania.
  Katika video pekee iliyonaswa Sportsmail, nyota huyo wa Brazil anaonekana akiondoka uwanjani baada ya kugombana na mr leo amchezaji mpya wa Barca, Nelson Semedo.
  Neymar amekuwa akihusishwa na kuondoka Barca kwa dau larekodi ya dunia kuhamia Paris Saint-Germain kwa Pauni Milioni 195, na sakata hili lmeibua maswali zaidi juu ya mustakabali wake Barca.
  Katika video hiyo, awali mambo yanaonekana kwenda vizuri, huku mshambuliaji huyo akienda kugombea mpira.
  Hata hivyo, Neymar na beki wa kulia, Semedo aliyesajiliwa kutoka Benfica wakageukiana na kuanza kuchimbiana mikwara baada ya kugombea mpira Benfica.
  Javier Mascherano haraka akaingia kwenda kuwaachanisha na Semedo akarudi nyuma, lakini Neymar akaonekana bado amekasirika huku akimtolea maneno beki huyo mpya huku akitulizwa Sergio Busquets.
  Pamoja na hayo akageuka na kuvua bifu kwa hasira kabla ya kupiga mpira kwenye langoni kwa hasira na kutoka nje ya Uwanja ambako mbele akapiga teke hewani na kutokomea zaidi.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NEYMAR AGOMBANA MAZOEZINI BARCA, AKASIRIKA ASUSA NA KUTOKOMEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top