• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 29, 2017

  MWANJALI NAHODHA MPYA SIMBA, WASAIDIZI BOCCO NA TSHABALALA…MKUDE APIGWA CHINI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  BEKI Mzimbabwe, Method Mwanjali ndiye Nahodha mpya wa kikosi cha Simba SC, akichukua nafasi ya kiungo Jonas Mkude.
  Mabadiliko hayo yamefanywa na benchi la ufundi la klabu ya Simba jana katika kambi ya Afrika Kusini chini ya kocha wake Mkuu, Mcameroon Joseph Omog. 
  Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Sunday Manara imesema kwamba Jonas Mkude atakaendelea kuwa mchezaji mwandamizi kwenye kikosi hicho kilicho maandalizi ya msimu mpya Afrika Kusini. 
  Katika mabadiliko hayo, 
  Method Mwanjali ndiye Nahodha mpya wa Simba SC, akichukua nafasi ya kiungo Jonas Mkude

  Kwenye mabadiliko hayo ya kawaida, benchi la ufundi pia limewateua Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita, beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na mshambuliaji mpya, John Raphael Bocco aa kuwa Manahodha wasaidizi. 
  Manara amesema Simba inamshukuru Nahodha wake wa msimu uliopita, Mkude ambaye pia nu mchezaji wake mwandamizi kwa kazi nzuri alioifanya muda wote alipokuwa Nahodha wa timu. 
  Kutoka kulia Erasto Nyoni, Salim Mbonde, Ally Shomary, John Bocco, Emmanuel Okwi na Mwinyi Kazimoto
  Kwa sasa kikosi cha Simba  kinaendelea na mazoezi na kila kitu kinakwenda vema huko kambini Eden Vale Johannesburg nchini Afrika kusini. 
  Wakati hu huo: Mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi leo ameanza mazoezi na wenzake Simba katika kambi ya Afrika Kusini baada ya kuripoti jana kufuatia kurejeshwa kikosi kwa mara ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MWANJALI NAHODHA MPYA SIMBA, WASAIDIZI BOCCO NA TSHABALALA…MKUDE APIGWA CHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top