• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 24, 2017

  MAN UNITED KUMKOSA BAILLY MECHI NA REAL UEFA SUPER CUP

  TIMU ya Manchester United imepata pigo katika safu yake ulinzi kuelekea mchezo wa UEFA Super Cup dhidi ya Real Madrid kutokana na adhabu ya Eric Bailly Ulaya kuongezwa. 
  Kamati ya NIdhamu ya UEFA imemfungia mechi tatu Bailly kwa kupigana uwanjani hadi kutolewa kwa kadi nyekundu mwishoni mwa mchezo wa Nusu Fainali ya Europa League kati ya Man United na Celta Vigo mwezi Mei.
  Bailly akaukosa mchezo wa ushindi wa 2-0 wa timu yake dhidi ya Ajax kwenye fainali ya Europa League hiyo ikiwa mechi yake ya kwanza kutumikia adhabu, lakini sasa atakuwa nje ya Super Cup na mechi ya ufunguzi ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

  Beki wa Manchester United, Eric Bailly ameadhibiwa na UEFA kwa tukio hili la Mei PICHA ZAIDI GONGA HAPA


  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alipigana na Facundo Roncaglia wa Celta Vigo katika sare ya 1-1 na Manchester United Uwanja wa Old Trafford. 
  Roncaglia pia alitolewa kwa nyekundu wakati Antonio Valencia alikuwa mwenye bahati kuepuka adhabu kama hiyo kutokana na kuwa sehemu ya tukio hilo.  
  United itamenyana na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Real Madrid Agosti 8 mjini Skopje, Macedonia kabla ya kuanza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Septemba baada ya droo kupangwa mjini Monaco Agosti 24.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED KUMKOSA BAILLY MECHI NA REAL UEFA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top