• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 25, 2017

  BEKI MGHANA ASAINI MIAKA MKITATU TIMU YA SAMATTA

  TIMU ya KRC Genk ya Ubelgiji imemsaini beki Mghana, Joseph Aidoo leo kwa mkataba wa miaka mitatu kuhamishia shughuli zake Uwanja wa Luminus Arena.
  Aidoo anayetokea Hammarby IF ya Sweden alipokuwa anacheza kwa mkopo, amesaini mkataba wa miaka mitatu wenye kipengele cha kuongezwa mwaka mmoja.
  Kisoka, Aidoo aliibukia Inter Allies ya kwao, Ghana kabla ya Januari mwaka 2016 kupelekwa kwa mkopo Hammarby IF kuanza kuizoea soka ya Ulaya.
  Beki kutoka Ghana, Joseph Aidoo ametambulishwa leo KRC Genk baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu

  Akiwa Hammarby, Joseph mwenye nguvu na mwili uliojengeka vyema kimazoezi, alicheza mechi 30 kwa kiwango cha juu na kufunga bao moja.
  Joseph ametambulishwa rasmi leo mchana Luminus Arena na kukabidhiwa jezi namba 45 Genk, ambayo ina mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Ally Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEKI MGHANA ASAINI MIAKA MKITATU TIMU YA SAMATTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top