• HABARI MPYA

    Monday, July 24, 2017

    NJOMBE MJI USIICHUKULIE POA, AZAM WAMEPIGWA 2-0

    Na Mwandishi Wetu, MAKAMBAKO
    WAGENI wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Njombe Mji FC leo wametoa onyo baada ya kuwafunga mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Azam FC mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amani, Makambako.
    Ikicheza kwa kushambulia kwa kasi, Njombe Mji ilifanikiwa kuifunika kabisa uwanjani timu ya bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake jioni ya leo na kusababisha washangiliwe muda wote wa mchezo na mashabiki wake.
    Mshambuliaji Mghana wa Azam FC, Yahya Mohammed akiwa juu kupiga mpira kichwa
    Wachezaji wa Njombe Mji FC wakimdhibiti mchezaji wa Azam FC leo
    Kama masihara, mshambuliaji Mnigeria wa timu hiyo, Adam Michael alianza kuifungia Njombe Mji dakika ya 35 na bao hilo likadumu hadi mapumziko.
    Kipindi cha pili, kocha Mromania wa Azam FC, Aristica Cioaba alibadilisha karibu kikosi kizima, lakini ajabu wakapachikwa bao la pili, lililofungwa na Raphael Siame dakika ya 80. 
    Tafrani iliibuka kidogo uwanjani baada ya Hussein Akilimali kuonekana kama ameokolea ndani ya mstari wa langoni krosi ya Mghana, Yahya Mohammed dakika ya 85, lakini baada ya refa kushauriana na msaidizi wake namba moja akajiridhisha halikuwa bao.
    Vikosi vilikuwa; 
    Azam FC; Metacha Mnata, Saleh Abdallah/Ramadhani Mohamed dk46, Abdul Haji/Iddi Kipagwile dk46, David Mwantika/Godfrey Elias dk46, Abdallah Kheri/Bruce Kangwa dk46, 
    Stanslaus Lwakatare/Aggrey Morris dk46, Abbas Kapombe/Yakubu Mohammed dk46, Masoud Abdallah/Frank Domayo dk46, Mudathir Yahya/Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dk46, Yahya Zayed/Bryson Raphael dk46 na Joseph Kimwaga/Yahaya Mohammed dk46.
    Njombe Mji FC; Daud Kissu/Erick Kaphoma dk46, Christopher Kizinde/Agathon Mapunda dk46, Said Abdallah/Remmy Mbuligwe dk46, Peter Mwangosi/Laban Kamboole dk46, Ahmed Tajdin/Hussein Akilimali dk46, Aden Chepa/Joshua John dk46, James Orash/Raphael Siame dk46, Behewa Sembwana/Awadh Salum dk46, Adam Baiko/Ditram Nchimbi dk46, Shaaban Kondo/Gwamaka Kilupe dk46 na Willy Mgaya/Juma Mpakala dk46.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NJOMBE MJI USIICHUKULIE POA, AZAM WAMEPIGWA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top