• HABARI MPYA

    Thursday, May 14, 2015

    WAZIRI WA MICHEZO IVORY COAST ATIMULIWA KASHFA YA ‘KUBWIA’ DOLA 800,000 ZA MASHUJAA WA AFCON

    Na Mwandishi Wetu, ABIDJAN
    WAZIRI wa Michezo wa Ivory Coast, Alain Lobognon (pichani kulia) amefukuzwa kazi jana, wiki moja baada ya Rais wa nchi hiyo, Alassane Ouattara kuagiza uchunguzi ufanyike juu ya wizi wa dola za Kimarekani 800 000, posho za wachezaji waliotwaa Kombe la Mataifa ya Afrika Februari mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
    Meneja Uhasibu wa taifa alifukuzwa wiki iliyopita, muda baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani kuanzisha uchunguzi wa kashfa hiyo.
    Wizira ya Michezo na Shirikisho la Soka wamekuwa wakinyoosheana vidole tangu mwezi uliopita baada ya wachezaji kuvujisha siri kwamba hawakulipwa posho zao.
    Baada ya kurejea kutoka AFCON, kila mchezaji aliahidiwa kupewa dola 97, 000 (dola 50, 000 wakipewa nyumba na dola 47, 000 fedha taslimu.
    Kocha Herve Renard alitakiwa kupewa dola 123, 000 wakati dola 490, 000 wangegawana wasaidizi wake katika benchi la Ufundi.
    Pamoja na hayo, kiungo wa VfB Stuttgart, Serey Die akasema mapema Aprili kwamba walipewa sehemu kidogo tu ya fedha hizo, wakati kocha huyo Mfaransa, Renard akathibitisha hajapata haki yake.
    Rais ameamua kuvalia njuga suala hilo baada ya kuona Wizara ya Michezo na FA wameshindwa kulipatia ufumbuzi. Tembo waliwafunga Ghana katika fainali kutwaa taji hilo la pili katika historia yao kwenye michuano hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI WA MICHEZO IVORY COAST ATIMULIWA KASHFA YA ‘KUBWIA’ DOLA 800,000 ZA MASHUJAA WA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top