• HABARI MPYA

    Friday, May 15, 2015

    NI SEVILLA NA DNIPRO FAINALI EUROPA LEAGUE 2015, WATALIANO WOTE NJE

    FAINALI ya Europa League 2015 itazikutanisha Sevilla na Dnipro ambayo usiku huu imeifunga 1-0 Napoli mjini Kiev na kuitupa nje kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza.
    Mashabiki wa timu ya nyumbani walivamia uwanani na vipeperushi mjini Kiev baada ya bao la kichwa la Yevhen Seleznyov kuitupa nje timu ya Rafa Benitez na kuipeleka fainali timu hiyo ya Ukraine.
    Seleznyov alifunga bao hilo pekee kwa kIchwa dakika ya 58 na Napoli inaishia hapa baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 Uwanja wa San Paolo wiki iliyopita.
    Dnipro itamenyana na Sevilla katika fainali ya Europa League mjini Warsaw Mei 27, mwaka huu.
    Sevilla imeingia fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-0, baada ya ushindi wa 2-0 usiku huu ugenini dhidi ya Fiorentina.
    Sevilla iliyoshinda 3-0 katika Nusu Fainali ya kwanza nyumbani, mabao yake leo usiku huu yamefungwa na Carlos Bacca na Daniel Carrico.
    A kiss is planted on Carlos Bacca after he scored Sevilla's opening goal at the Artemio Franchi stadium
    Busu la uopendo kwa Carlos Bacca baada ya kuifungia bao pekee la Sevilla Uwanja wa Artemio Franchi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI SEVILLA NA DNIPRO FAINALI EUROPA LEAGUE 2015, WATALIANO WOTE NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top