• HABARI MPYA

    Friday, May 01, 2015

    STURRIDGE AENDA MAREKANI KUJUA KAMA ATAHITAJI 'KISU' TENA

    MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Daniel Sturridge amekwenda kumuona mtaalamu mjini Boston, Marekani ili kujua kama atahitaji upasuaji kutatua tatizo lake la paja.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa England amecheza mara mbili tu tangu aumie katika mechi dhidi ya Manchester United Machi 22 na kocha Brendan Rodgers wiki iliyopita alielezea wasiwasi wake kama mshambuliaji huyo atacheza tena msimu huu.
    Sasa hali inaelekea kuwa hivyo, baada ya Sturridge kwenda kumuona Dk Peter Asnis kujua mustakabali wa maumivunyake.
    Daniel Sturridge has gone to see a US specialist to determine whether he needs surgery on his hip
    Daniel Sturridge amekwenda Marekani kujua kama atahitaji upasuaji wa paja lake
    Sturridge also spent time in Los Angeles as he worked on recovering from a thigh problem
    Sturridge pia aliwahi kwenda Los Angeles, Marekani kufanya mazoezi ya kutafuta nafuu ya maumivu yake

    Hii ni mara ya pili kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, Sturridge anapelekwa Marekani kwa sababu ya maumivu yake. 
    Desemba mwaka jana alikuwa Los Angeles na baadaye Boston kujifua kutafuta ahueni ya maumivu hayo yaliyomuweka nje kwa miezi mitano.
    Rodgers sasa atalazimika kutoa fedha kununua mshambuliaji mwingine kwa ajili ya msmu ujao, kutokana na matatizo ya Sturridge. Nyota wa PSV Eindhoven, Memphis Depay ndiye mlengwa wake wa kwanza na mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uholanzi inasemekana yuko tayari kuhamia Anfield.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STURRIDGE AENDA MAREKANI KUJUA KAMA ATAHITAJI 'KISU' TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top