• HABARI MPYA

    Wednesday, May 13, 2015

    NSIMBE NA WENZAKE WAPELEKWA TIMU B AZAM FC, STEWART AJA NA BENCHI ZIMA LA UFUNDI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    BENCHI lote la Ufundi la sasa la Azam FC litahamishiwa katika timu za vijana za klabu hiyo, maarufu kama Azam Academy na kocha Muingereza Stewart John Hall anakuja timu A na timu kamili ya makocha wa kufanya nao kazi.
    Kocha Muingereza Stewart Hall anarejea kazini Azam FC na benchi lake zima la ufundi 

    REKODI YA GEORGE NSIMBE AZAM FC 

    Azam FC 1-0 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
    Azam FC 1-0 Ndanda FC (Ligi Kuu)
    Azam FC 1-0 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Azam FC 1-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
    Azam FC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
    Azam FC 0-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
    Azam FC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
    Azam FC 4-0 Stand United (Ligi Kuu)
    Azam FC 1-2 Simba SC (Ligi Kuu)
    Azam FC 2-1 Yanga SC (Ligi Kuu)
    Azam FC 0-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu) 
    Hall ambaye awali aliifundisha Azam FC kwa awamu mbili, anakuja na Kocha Msaidizi, kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili na kocha wa makipa kuanza kuiandaa timu kwa ajili ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati.
    Michuano hiyo maarufu kama Kombe la Kagame inatarajiwa kuanza Julai 11 mjini Dar es Salaam na baada ya Azam FC kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu msimu huu, imevunja benchi la Ufundi.
    Aliyekuwa kaimu kocha Mkuu, Mganda George ‘Best’ Nsimbe na timu yake nzima, Dennis Kitambi, Iddi Abubakar kocha wa makipa na Meneja Jemadari Said wanakwenda Azam Akademi.
    BIN ZUBEIRY inafahamu baadhi ya watu kutoka benchi la sasa la Ufundi la Azam FC wataondolewa moja kwa moja, lakini wengi wao watapewa majukumu Azam Akademi.
    Tangu amerithi mikoba ya Mcameroon, Joseph Marius Omog Machi mwaka huu, Nsimbe ameiongoza Azam FC katika mechi 11, akishinda sita, sare nne na kufungwa moja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NSIMBE NA WENZAKE WAPELEKWA TIMU B AZAM FC, STEWART AJA NA BENCHI ZIMA LA UFUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top