BONDIA Manny Pacquiao amegoma kumtaja mpinzani wake afuataye na kusema kwa sasa anafikiria kupona tu bega lake alilloumia akijiandaa kupigana na Floyd Mayweather.
Pamoja na kupoteza pambano hilo kwa pointi mapema mwezi huu, Pacquiao alikuwa mwenye tabasamu wakati anawasili nyumbani.
Mbabe huyo mwenye umri wa miaka 36, alirejea nyumbani, Ufilipino kwa mara ya kwanza baada ya pambano lake la karne na kusalimia umati wa watu mjini Manila.
Nyota huyo wa Ufilipino alirejea nyumbani siku nne tangu afanyiwe upasuaji mjini Los Angeles, huku mkono wake umekuwa umefungwa.
Bondia huyo mwenye makonde mazito tishio kwa wapinzani, ameposti kwenye akaunti yake ya Instagram kumtakia heri mkewe ya miaka ya mitano 15 yao.
Pacquiao alikutana na mkewe, Jinkee na mtoto wake mdogo wa kiume, Israel Uwanja wa Ndege na akazungumza na Waandishi wa Habari baada ya kutua Manila.
Akasema kwa sasa anaelekeza fikra zake kwenye kupata ahueni ya maumivu yake na hakutaka kusema atapigana na nani katika pambano lijalo, ingawa ana matumaini ya kurejea ulingoni mwakani.
"Kwa sasa sizungumzii kuhusu hiyo, kuhusu pambano langu lijalo,"amesema akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Manila. "Fikra zangu ni kupata ahueni na kuwa sawa. Daktari amesema nitakuwa sawa kwa asilimia 100,".


.png)
0 comments:
Post a Comment