• HABARI MPYA

    Friday, May 15, 2015

    SIMBA SC YATUPA NDOANA ZAKE KWA BEKI TEGEMEO RWANDA, TENA KINDA TU

    Na Princess Asia, DAR ES SAALAM
    SIMBA SC imetupa ndoana zake kwa Emery Bayisenge wa APR ya Rwanda, lakini kumpata kazi ipo.
    Bayisenge, beki hodari wa kati mwenye umri wa miaka 21 tu, ni tegemeo la Rwanda kuelekea michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika CHAN mwakani, inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
    Kwa sababu hiyo, Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) halitapenda kukipoteza kisiki hicho kabla ya CHAN ya mwakani, ambayo wao watakuwa wenyeji. 
    Simba SC inamtaka Emery Bayisenge, lakini kikwazo ni FERWAFA inayotaka kumtumia katika CHAN mwakani

    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ni shabiki mkubwa wa beki huyo na BIN ZUBEIRY inafahamu yuko katika jitihada kubwa za kuhakikisha anamhamishia Msimbazi.
    Bayisenge mwenyewe kwa mvuto wa maslahi na hamu yake kubwa ya kucheza Tanzania, yuko tayati kutua Simba SC- lakini FERWAFA ndiyo kikwazo. 
    Bayisenge ambaye kabla ya APR alichezea Amagaju na Isonga, amekuwa akiichezea Amavubi tangu mwaka 2011.
    CHAN ijayo inatarajiwa kufanyika Rwanda kuanzia Januari 16 hadi Februari 7 ikishirikisha jumla ya timu 16.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YATUPA NDOANA ZAKE KWA BEKI TEGEMEO RWANDA, TENA KINDA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top