// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); POLISI MARA YAZUIWA KUCHEZA UWANJA WA KARUME MUSOMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE POLISI MARA YAZUIWA KUCHEZA UWANJA WA KARUME MUSOMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, January 14, 2015

    POLISI MARA YAZUIWA KUCHEZA UWANJA WA KARUME MUSOMA

    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeizuia timu ya Polisi Mara kutumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma kwa mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuanzia leo mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
    Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na matukio ya vurugu na uvunjifu wa amani ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mechi za FDL zinazochezwa kwenye uwanja huo, ikiwemo ile ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Mwadui ya Shinyanga ambapo waamuzi walipigwa.

    Kamati zinazohusika zitakutakana hivi karibuni kupitia matukio yote ya utovu wa nidhamu kwenye FDL, na hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika ikiwemo na viwanja ambavyo vimekuwa na sifa ya vurugu.
    Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vina wajibu wa kutoa ulinzi wa kutosha viwanjani wakati wa mechi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: POLISI MARA YAZUIWA KUCHEZA UWANJA WA KARUME MUSOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top