• HABARI MPYA

  Thursday, January 15, 2015

  JOHN BOCCO ATIMKIA ALGERIA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ yuko mjini Ain Fakroun, Algeria kwa ajili ya mipango ya kujiunga na klabu ya Chabab Riadhi Baladiyat, maarufu kama CRB. Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Bocco yuko huko kwa siku kadhaa baada ya kwenda mwanzoni mwa wiki kufanya mipango ya kujiunga na timu inayovalia jezi za rangi nyeusi na nyeupe. 
  Kawemba amesema timu hiyo ya Daraja la Kwanza Algeria, maarufu kama Professionnelle 2 inataka kumnunua moja kwa moja Bocco, lakini ilitaka kumuona kwanza.
  Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco wakati alipokuwa Supersport ya Afrika Kusini

  “Ilikuwa tangu jana tupate majibu yao baada ya kumuona na kuzungumza naye, lakini tumeona kimya, hivyo tunawapa muda zaidi hadi kesho jioni kabla hatujaamua cha kufanya,”amesema Kawemba. 
  Msimu wa 2012–13, CRB Ain Fakroun ilishika nafasi ya kwanza katika Professionnelle 2 na kufanikiwa kupanda Ligi Kuu ya Algeria ijulikanayo kama Professionnelle 1 kwa mara ya kwanza, kabla ya kushuka tena.
  John Raphael Bocco aliyezaliwa Agosti 5, mwaka 1989 amewahi kufanya majaribio Afrika Kusini na Israel, ambako licha ya kuelezwa alifuzu, lakini biashara haikufanyika.
  Awali, Bocco alifanya majaribio kwa wiki kadhaa katika klabu ya Ligi Kuu Israel mwaka 2010 na baadaye Afrika Kusini katika klabu ya Supersport United.
  Bocco alifuzu Supersport baada ya wiki mbili, lakini Azam FC ikagoma kumuuza kwa sababu ya dao dogo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOHN BOCCO ATIMKIA ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top