• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 01, 2013

  EVELYNE NDIYE REDD'S MISS UNI COLLEGE 2013

  Redd's Miss Uni College 2013, Evelyne Mathew (katikati) akiwa na washindi wenzake wa pili hadi wa tano baada ya kutajwa matokeo usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Billicanas, Dar es Salaam. 
  Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JUNI 1, 2013 SAA 1:15 ASUBUHI
  MWANAFUNZI wa Chuo cha Bandari, Evelyne Mathew (20) usiku wa kuamkia lepo ameibuka Redd’s Miss Uni College Temeke baada ya kuwabwaga wenzake 12 katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Club Billicanas, Dar es Salaam.
  Evelyne katika vazi la ufukweni

  Katika shindano hilo lililoshirikisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali Temeke, nafasi ya pili ya ilikwenda kwa Pheibe Urio anayesoma Chuo cha Bandari pia na Nyangeta Kuboja anayesoma Chuo cha Kimataifa cha Kampala (KIA), tawi la Dar es Salaam.
  Nafasi ya nne ilikwenda kwa Subirs Ally na wa tano alikua Nelly Twarane, wote chuo cha Bandari.  
  Washiriki wengine ambao hawakuingia tano bora ni Paulina Komba, Joanita Revocatus, Catherine Chriss, Irene Jisla, Mary Mayemba, Christine Kwidoya, Halima Shaaban na Agnes Sylvester.
  Mshindi wa kwanza ameondoka na zawadi ya Sh. 300, 000, wa pili 200,000 na wa tatu 100,000 na wote wamesonga mebele kwenye Miss Vyuo Dar es Salaam.
  Mshindi wa nne na wa tano ambao wanapata Sh. 50,000 kila mmoja, wanaungana na wale ambao hawakuingia tano bora kuyaaga mashindano ya Redd’s Miss Tanzania mwaka huu.     
  Nyota wa R&B, Ben Pol alikonga nyoyo za mashabiki kwa nyimbo zake mbalimbali kwenye ukumbi huo kabla ya kutajwa washindi.
  Evelyne akilia baada
  ya kushinda

  Baada ya kutajwa washindi, wanafunzi wa Chuo cha Bandari walivamia jukwaa kumpongeza mwenzao kwa ushindi huo.
  Ilkuwa ni furaha tupu jukwaani na shangwe za kugalagala, hadi ikabidi walinzi wa Billicanas wapande jukwaani kuondoa watu ili kulinda usalama wa warembo.
  Wakati huo, warembo wengine walioshika nafasi kuanzia ya pili, walikuwa wameketi nyuma wakishuhudia mwenzao wakipongezwa.
  Watazamani waliridhika na matokeo pia, kwani Evelyine tangu mwanzo alionekana kuwazidi wenzake vigezo vya ushindi na hivyo ushindi wake ulitarajiwa na wengi.
  Evelyne akiwa ameanguka chini kwa furaha ya kilio cha ushindi

  Dj Ibra wa Club Billicanas akimshuhudia Jaji Salma Dakota akitangaza washindi

  Shoo ya ufunguzi, Evelyne mbele kushoto
    


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: EVELYNE NDIYE REDD'S MISS UNI COLLEGE 2013 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top