• HABARI MPYA

    Thursday, April 11, 2013

    TRA YAIPA SIKU 10 TFF KULIPA DENI LA SH MILIONI 573, VINGINEVYO...

    Wazee wa Madeni; Rais wa TFF, Leodegar Tenga

    Na Mahmoud Zubeiry
    MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewapa siku 10 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulipa deni la Sh. 573, 525, 673.8 kuanzia Jumatatu au wakate Rufaa.
    Kwa mujibu wa vyanzo kutoka TRA, Maofisa wa Mamlaka hayo walifanya tathmini Machi 14, mwaka huu kutokana na ukaguzi wa hesabu za shirikisho hilo na kukuta wana deni linalotokana na kodi za Lipa Kadiri Unavyoingiza (PAYE) na Ongezeko la Thamani (VAT) la jumla ya Sh. 573, 525,673.8.
    Kufuatia hali hiyo, TRA ikawaandikia barua TFF ikiwataka walipe ndani ya siku 10 kuanzia Jumatatu au wakate Rufaa.
    Alipoulizwa na BIN ZUBEIRY leo kuhusu suala hilo, Katibu wa TFF, Angetile Osiah Malabeja amesema kwamba hawezi kulizungumzia suala hilo, kwa sababu walikwishakubaliana na Serikali litazungumziwa na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara.  
    “Sisi tulikubaliana na Wizara kwamba tusilizungumzie suala la deni la kodi za mishahara ya makocha, na atakayelizungumzia ni Waziri,”alisema Angetile.
    Mwishoni mwa mwaka jana, TRA ilizifunga akaunti za udhamini za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kama shinikizo kwa TFF kulipa makato ya kodi za mishahara ya makocha wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars tangu kipindi cha Mbrazil Marcio Maximo na Wadenmark, Jan Poulsen na huyu wa sasa, Kim Poulsen ambayo ilikuwa ni Sh 157,407.968.00. 
    Kwa hali hiyo, TFF iliomba msaada wa serikali ambao ndio walipaji wa mishahara ya makocha wa Taifa Stars
    Hata hivyo, deni la sasa la TFF kwa TRA ni zaidi ya nusu na inaonekana halitokani tu kodi za mishahara ya makocha wa Taifa Stars.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TRA YAIPA SIKU 10 TFF KULIPA DENI LA SH MILIONI 573, VINGINEVYO... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top