// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); UCHAGUZI TFF WAPIGWA 'TEKE' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE UCHAGUZI TFF WAPIGWA 'TEKE' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, November 17, 2012

    UCHAGUZI TFF WAPIGWA 'TEKE'

    Wakili Alex Mgongolwa

    Na Mahmoud Zubeiry
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema kwamba Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa shirikisho hilo utafanyika Februari 16 na 17 mwakani, badala ya Desemba mwaka huu kufuatia Kamati ya Utendaji kuafiki mapendekezo ya marekebisho ya Katiba katika kikao chake cha Novemba 3, mwaka huu 2012.
    Taarifa iliyotumwa kwa BIN ZUBEIRY na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF, Wakili Alex Mgongolwa imesema kwamba baada ya kutafakari mapendekezo hayo, Kamati ya Utendaji ya TFF imeamua kuifanyia marekebisho Katiba ya shirikisho hilo kama iliyopendekezwa.
    “Kwa vile mapendekezo mawili kati ya matatu ya ya marekebisho ya Katiba yana uhusiano na Uchaguzi Mkuu wa TFF, ipo haja ya marekebisho hayo kufanyika kabla ya kutangazwa kwa Mkutano Mkuu wa TFF na kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF,”imesema taarifa ya Mgongolwa.
    Aidha, Mgongolwa amesema kwa vile TFF haina uwezo wa kuitisha mikutano mikuu miwili – Mkutano Mkuu Maalum kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ya TFF; na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi – katika kipindi kifupi kijacho, marekebisho ya Katiba yafanywe kwa njia ya Waraka (“Circular Resolution”).
    “Waraka huo (“Circular Resolution”) uwe umeshatayarishwa na Sekretariati ikishirikiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ifikapo tarehe 15 Novemba 2012 na ukabidhiwe kwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaowakilisha Kanda za TFF ambao watahakikisha kuwa  kila Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Kanda husika anapata fursa ya kutoa ridhaa yake,”imesema taarifra ya Mgongolwa.
    Aidha, wakili huyo ameagiza zoezi la kupata ridhaa ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu liwe limemalizika katika kipindi cha siku 21 na kwamba kikao kinachofuata cha Kamati ya Utendaji Desemba 15, mwaka huu kiwe kwa madhumuni ya kupokea taarifa ya zoezi hili na kufanya matayarisho ya Mkutano Mkuu.
    “Katiba ya TFF inaelekeza kuwa taarifa ya Mkutano Mkuu itolewe kwa wanachama wake angalau siku 60 (“notice period”) kabla ya Mkutano. Hivyo Kamati ya utendaji inatarajia kuwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utafanyika Jumamosi na Jumapili ya tarehe 16 na 17 na Februari 2013,”.
    Amesema Kamati ya Utendaji ya TFF inasisitiza kuwa utaratibu huo umeamuliwa kutokana na TFF kutokuwa na uwezo wa kifedha wa kutayarisha mikutano mikuu miwili katika kipindi kifupi kijacho na kwamba kinyume chake ni kuchelewa zaidi kufanyika kwa Mkutano Mkuu, jambo ambalo hawana budi kuliepuka.
    Amesema Kamati ya Utendaji ya TFF inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na wadau wa soka kwa jumla ili kufanikisha zoezi hilo na hatimaye kufanikisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa TFF.
    Katika kikao chake cha Novemba 3, mwaka huu, Kamati ya Utendaji ya TFF ilipokea taarifa ya mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ikitakiwa kuongeza kipengele kinachohusu “Club Lincencing” kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) katika waraka wake unaowataka wanachama wote wa CAF, ikiwemo TFF, kuhakikisha kuwa kipengele hicho kinaingizwa katika katiba zao.
    Kutokana na ushauri na maagizo ya FIFA, TFF inatakiwa kuunda wa Kamati ya Rufaa ya Uchanguzi (“Elections Appeals Committee”) na kuondokana na utaratibu iliyonao hivi sasa, ambao Kamati ya Rufaa (“Appeals Committee”) inajigeuza na kuwa Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi wakati wa mchakato wa uchaguzi wa TFF.
    Pendekezo lingine ni kuindoa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais wa TFF pamoja na kutamka kuwa Wawakilishi wa klabu za Ligi Kuu katika Kamati ya Utendaji watachaguliwa moja kwa moja na klabu zenyewe.
    Hiyo inatokana na azimio la Mkutano Mkuu uliopita la kuruhusu uundwaji wa chombo huru cha kusimamia Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza pamoja na kupitishwa kwa Kanuni zinazokiongoza chombo hicho kama zilivyopendekezwa na klabu za Ligi Kuu na kupitishwa na Kamati ya Utendaji ya TFF.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: UCHAGUZI TFF WAPIGWA 'TEKE' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top