Van Persie

Tetesi za Alhamisi magazeti ya Ulaya

WENGER AFARIJIKA, VAN PERSIE HAONDOKI

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger anajiamini Nahodha wake, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28, atabakia Arsenal, licha ya kubakiza miezi 12 tu katika mkataba wake na washika Bunduki hao wa London.
KOCHA wa Newcastle United, Alan Pardew anajiandaa kukutana na mshambuliaji Demba Ba, mwenye umri wa miaka 27, wiki hii kujadili mustakabali wa mpachika mabao huyo wa kimataifa wa Senegal.
Martin Skrtel
Martin Skrtel anatakiwa Man City
KLABU ya Manchester City inaandaa dau la pauni Milioni 20 kumnasa beki wa Liverpool, Martin Skrtel, mwenye umri wa miaka 27, kama mbadala wa beki Thiago Silva ambaye wameamua kuachana naye.
KIPA wa Tottenham, Heurelho Gomes, mwenye umri wa miaka 31, anataka kubaki katika klabu hiyo licha ya kufukuzwa kwa klocha Harry Redknapp.
KLABU ya Norwich City imejitokeza na nia ya kumsajili kipa wa England na Birmingham, Jack Butland, mwenye umri wa miaka 19.
KLABU ya Swansea inataka kumsajili kiungo wa PSV Eindhoven, Otman Bakkal, mwenye umri wa miaka 27.

SAHA AMPIGIA DEBE BLANC SPURS

Laurent Blanc
Laurent Blanc 
MSHAMBULIAJI wa Ufaransa, Louis Saha anaamini kocha wa sasa Ufaransa, Laurent Blanc, mwenye umri wa miaka 40, angeng'ara katika klabu ya Tottenham ikiwa angerithi mikoba ya Harry Redknapp.
KLABU ya Rangers imeonyesha nia ya kuinunua klabu ya Daraja la Kwanza, Bury hivyo wanaweza kuhamia England.

ROONEY AFUKUZIA 'AFRO' LA ANDY CARROLL

MSHAMBULIAJI wa England, Wayne Rooney amesema anataka kukuza nywele zake ziwe kama za mshambuliaji mwenzake wa England, Andy Carroll.