• HABARI MPYA

  Wednesday, April 10, 2019

  SINGIDA UNITED YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA KMC LIGI KUU LEO UWANJA WA NAMFUA

  Na Mwandishi Wetu, SINGIDA
  TIMU ya Singida United imeshindwa kutumia vyema Uwanja wa nyumbani, Namfua mkoani Singida baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na KMC ya Kinondoni mjini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jiioni ya leo.
  Matokeo hayo yanayoiongezea pointi moja kila timu yanamaanisha, KMC inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 32 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya sita, wakati Singida United inayofikisha pointi 40 katika mechi ya 33 inapanda hadi nafasi ya 10 kutoka ya 13.
  Mshambuliaji Habib Hajji Kiyombo anayeripotiwa kutakiwa na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini alianza leo na akakosa bao la wazi Uwanja wa Namfua.

  Na kilichowasaidia zaidi KMC walio chini ya kocha Mrundi, Ettienne Ndayiragijje leo ni mchezo wao wa kujihami zaidi na kushambulia kwa kushitukiza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA KMC LIGI KUU LEO UWANJA WA NAMFUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top