• HABARI MPYA

    Tuesday, April 09, 2019

    DK MSOLLA ACHUKUA FOMU KUWANIA UENYEKITI YANGA, MBUNGE WA ILEJE ATAKA UMAKAMU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa zamani wa Taifa Stars, Dk Mshindo Msolla ni miongoni mwa watu watatu waliochukua fomu za kuwania Uenyekiti katika klabu ya Yanga katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Mei 5, mwaka huu – wengine wakiwa ni Elias Mwanjala na Lucas Mashauri.
    Watatu hao wanaungana na Dk. Jonas Benedict Tiboroha, Mbaraka Hussein Igangula na Erick Ninga waliochukua fomu awali kabla ya uchaguzi huo kuahirishwa.
    Nafasi ya Makamu Mwenyekiti waliochukua na kurudisha fomu ni Katibu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Wilfred Mwakalebela, Samuel Lukumay, Thobias Lingalangala na Mbunge wa jimbo Ileje (CCM) Mheshimiwa, Janet Zebedayo Mbena.

    Dk Mshindo Msolla (kulia) amejitokeza kuwania Uenyekiti Yanga katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Mei 5, mwaka huu

    Hao wanaungana na Yono Kevela, Titus Eliakim Osoro na Salum Magege Chota waliopitishwa awali kuwania nafasi hiyo kabla ya uchaguzi huo kuahirishwa.
    Katika nafasi za Ujumbe waliochukua fomu ni Ally Sultan Hemed ‘Chota’, Saad Mohamed Khimji, Hassan Yahya Hussein, Siza Augustino Limo, Dominick Albinus, Seko Jihadhari Kingo, Hamad Islam, Cyprian Musiba na Mhandisi Leonard Marangu.
    Wengine ni Nassor Matuzya, Abdallah Mussa Chikawe, Hussein Nyika, Rodgers Gumbo, Said Rashid Omar Ntimizi, Paulina Conrad, Elias Mkumbo, Seif Mwaitenda, Seif Hassan Seif na Haruna Hussein Batenga.   
    Na hao wanaungana na wengine 16 Hamad Ally Islam, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvester Haule, Salim Seif, Shafil Amri, Said Kambi, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omar Msigwa, Arafat Ally Hajji, Frank Kalokola, Ramadhani Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopher Kashiririka na Athanas Peter Kazige waliopitishwa awali.
    Uchaguzi huu unakuja baada ya viongozi wote waliochaguliwa Juni 11 mwaka 2016 kujiuzulu kwa wakati na sababu tofauti.
    Waliojiuzulu ni aliyekuwa Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wanne, Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi, Hashim Abdallah, Siza Augustino Lymo, Tobias Lingalangala, Samuel Lukumay na Hussein Nyika.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DK MSOLLA ACHUKUA FOMU KUWANIA UENYEKITI YANGA, MBUNGE WA ILEJE ATAKA UMAKAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top