• HABARI MPYA

  Tuesday, May 16, 2017

  SHANGWE ZA UBINGWA YANGA KUANZA LEO?

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC wanaweza kuanza kushangilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo, iwapo wataifunga Toto Africans Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
  Ushindi katika mchezo wa leo, utawafanya mabingwa hao watetezi wafikishe pointi 68 katika mechi ya 29 na ambazo zinaweza kufikiwa tu na wapinzani wao katika mbio hizo, Simba SC wakishinda mechi yao ya 30 na ya mwisho msimu huu dhidi ya Mwadui.
  Lakini kinachoweza kuwafanya Yanga waanze kushangilia ubingwa leo hata kabla ya kuingia kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mbao FC wiki ijayo Mwanza ni idadi kubwa ya mabao wanayowazidi Simba.
  Yanga imefunga mabao 56, imefungwa 13 maana yake ina mabao 43 ukitoa 13 ya kufungwa, wakati Simba imefunga mabao 48 na imefungwa 16 – maana yake ina mabao 32 ukitoa 16 ya kufungwa.
  Na Yanga leo itabidi wafumbe macho kuifunga Toto Africans iliyo hatarini kushuka daraja, kwani kihistoria timu hiyo ya Mtaa wa Kishamapanda, Mwanza ni ‘Mtoto wa damu’ wa timu ya Jangwani, Dar es Salaam.  
  Ni mechi ya mgongano wa maslahi ambayo itaweka pembeni undugu baina ya timu hizo na kila mmoja kuingia uwanjani kupigania maslahi yake, Yanga ikiwania ubingwa na Toto Africans ikijaribu kuepuka kushuka Daraja.
  Toto Africans ina pointi 29 katika nafasi ya 15 baada ya kucheza mechi 28 ikiwa juu ya JKT Ruvu imayoshika mkia kwa pointi zake 23 za mechi 29 na ambayo imekwishashuka Daraja.
  Juu yake kuna Ndanda FC ya Mtwara yenye pointi 30 za mechi 29, sawa kabisa na Mbao FC ya mwanza wakati African Lyon ina pointi 31 za mechi 29 na Maji Maji FC pointi 32 za mechi 29 pia.   
  Toto Africans inajivunia mchezo mwingine mmoja dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya mchezo wa leo, ambao kama itashinda na wapinzani wake, Ndanda FC na Mbao FC wakateleza kwenye mechi zao za mwisho basi itabaki Ligi Kuu ‘kwa bahati mno’.
  MECHI ZA KUHITIMISHA MSIMU WA LIGI KUU

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHANGWE ZA UBINGWA YANGA KUANZA LEO? Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top