• HABARI MPYA

  Tuesday, May 16, 2017

  MALINZI AMRUDISHIA ASANTE DK MWAKYEMBE MAVITU YA SERENGETI BOYS GABON

  Na Alfred Lucas, LIBREVILLE
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amemrudishia asante Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harisson Mwakyembe kutokana na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kuanza na sare dhidi ya timu ngumu, Mali katika Fainali za Afrika.
  Serengeti Boys jana iligawana pointi na mabingwa watetezi, Mali katika mchezo wa kwanza wa Kundi B Fainali za Mataifa ya Afrika Uwanja wa l’Amitie Sino mjini Libreville, Gabon na kutikana na hilo, Malinzi akasema; “Haya yote kayafanya Dk. Harrison Mwakyembe.”
  Akizungumza mjini hapa leo, Malinzi amesema: “Ujumbe wa kuitakia kheri Serengeti Boys ulitolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo umeisukuma timu hiyo kufanya vema.
  Waziri Mwakyembe ndiye aliyewakabidhi bendera Serengeti Boys wakati wanaondoka Dar es Salam

  “…Ndiyo, timu imekuwa ikijindaa physical, lakini kupata neno la mzazi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Dk. John Magufuli kupitia Waziri wa Michezo, Mheshimiwa Mwekyembe liliwatia nguvu vijana kufanya vema na kuzuia Mali kuIshinda Serengeti.”
  Vyombo vya habari vya hapa Libreville, vimesema Serengeti Boys ni timu ya kuchungwa mara baada ya matokeo ya jana dhidi ya Mabingwa watetezi - Mali ambayo pia ni makamu bingwa katika Kombe la Dunia la FIFA kwa vijana chini ya miaka 17.
  Vyombo vya habari vya hapa vimesema ni matokeo mazuri na hata ya kushangaza kwani Mali ni timu ambayo hakuna timu inapenda kukutana nayo.
  “La kushangaza kwa timu ya Tanzania ambayo pamoja na Angola zina vijana wanaoonekana kuwa na umri mdogo kulinganisha na timu za Afrika Magharibi, ni uwezo wao wa kubaki kwenye mpango wa mchezo hata walipokumbana na mawimbi makali,” limesema gazeti la Le Moniour.
  Serengeti Boys imeanza kufuatiliwa na kuangalia matokeo yake ya mechi za nyuma na kuonekana imepoteza mechi chache za kimataifa na kuzifunga timu kama za Afrika Kusini, kutoka sare na Korea Kusini na Marekani katika michuano mbalimbali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALINZI AMRUDISHIA ASANTE DK MWAKYEMBE MAVITU YA SERENGETI BOYS GABON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top