• HABARI MPYA

  Wednesday, February 15, 2017

  SIMBA NA AFRICAN LYON KUKIPIGA KESHO TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC itamenyana na African Lyon kesho katika Raundi ya Sita ya Kombe la Shirikisho la Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Awali, mchezo huo ulipangwa kufanyika Machi 1, mwaka huu lakini ulirudishwa nyuma kwa sababu za kiufundi kutoka timu zote mbili.
  Michuano ya raundi hiyo ya sita, itaendelea tena Februari 24, mwaka huu kwa michezo minne kuchezwa kwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja tu utakaochezwa saa 1.00 jioni.
  Michezo ya siku hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mechi nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.
  Jumapili Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Machi 7, mwaka huu Yanga SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA AFRICAN LYON KUKIPIGA KESHO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top