• HABARI MPYA

  Tuesday, February 14, 2017

  SIMBA, AFRICAN LYON RAUNDI YA 6 AZAM SPORTS FEDERATION KUCHEZA ALHAMISI FEBRUARI 16

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAUNDI ya Sita ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) 2016/17, itaanza Februari 16, 2017 badala ya Februari 24, mwaka huu.
  Mchezo huo awali ulipangwa kufanyika Machi mosi, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja kabla ya kuendelea tena Februari 24, mwaka huu kwa michezo minne kuchezwa kwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja tu utakaopigwa saa 1.00 jioni.
  Michezo hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na TFF, itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mechi nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea ilihali Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.
  Jumapili Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA, AFRICAN LYON RAUNDI YA 6 AZAM SPORTS FEDERATION KUCHEZA ALHAMISI FEBRUARI 16 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top