• HABARI MPYA

  Friday, February 03, 2017

  NGOMA AREJEA YANGA IKIIVAA STAND LEO, ANAANZA NA CHIRWA MABAO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga, George Lwandamina leo amewaanzisha pamoja Mzambia mwenzake Obrey Chirwa na Mzimbabwe, Donald Ngoma katika safu ya ushambuliaji kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Stand United.
  Yanga wanaikaribisha Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo katika mchezo ambao wanahitaji kulipa kisasi cha kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza.
  Donald Ngoma anaanza leo dhidi ya Stand United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  Na Lwandamina aliye katika msimu wake wa kwanza Yanga baada ya kumpokea Mholanzi, Hans van der Pluijm Novemba mwaka jana amerudia ‘ukiuta’ ule ule uliowezesha timu kushinda 2-0 dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga Jumapili.
  Kwa ujumla, kikosi cha Yanga leo kipo hivi; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondan, Justin Zulu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Ngoma, Chirwa na Haruna Niyonzima.
  Stand United; Sebastain Stanley, Jacob Massawe, Erick Mulilo, Adeyum Ahmed, Revocatus Richard, Ibrahim Job, Abdulaziz Makame, Adam Salamba, Frank Khamis, Abasalim Chidiebele na Suleiman Kassim ‘Selembe’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGOMA AREJEA YANGA IKIIVAA STAND LEO, ANAANZA NA CHIRWA MABAO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top