• HABARI MPYA

  Sunday, February 19, 2017

  MAMELODI WAITWANGA MAZEMBE NA KUBEBA SUPER CUP YA CAF

  TIMU ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini usiku wa jana imetwaa taji la Super Cupa Afrika baada ya kuwafunga bao 1-0 vigogo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa Loftus Versfeld mjini Pretoria.
  Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, Ricardo Nascimento kwa penalti dakika ya 83, baada ya Hlompho Kekana kuangushwa kwenye boksi. 
  Mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa, maarufu kwa jina ka utani 'Wabrazil' walistahili ushindi huo kutokana na kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo uliowakutanisha na mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika.
  Nafasi nzuri zaidi Mazembe walishindea kuitumia katika mchezo huo ilikuwa ni wakati mshambuliaji Ben Malango alipobaki peke yake na kipa Mganda Denis Onyango, lakini akipiga mpira ukagonga mwamba wa juu kulia.
  Mshambuliaji huyo wa Mazembe akafanikiwa kuupata mpira uliorudi na akajitengeneza vizuri kupiga tena, lakini Onyango akawa tayari amekwishajipanga na kuuchupia pembezoni ma lango kuokoa.
  Kikosi cha Sundowns kilikuwa; Denis Onyango, Thapelo Morena, Wayne Arendse, Ricardo Nascimento, Tebogo Langerman, Tiyani Mabunda, Hlompho Kekana, Themba Zwane/Sibusiso Vilakazi dk90+3, Anthony Laffor/Bangaly Soumahoro dk86, Khama Billiat/Anele Ngcongca dk90+2 na Percy Tau
  Mazembe: Sylvain Gbohouo, Djos Issama, Joel Kimwaki, Salif Coulibaly, Jean Kasusula, Nathan Sinkala, Daniel Adjei, Rainford Kalaba/Adama Traore dk80, Solomon Asante, Ben Malango, Meschak Elia/Tresor Mputu dk58.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMELODI WAITWANGA MAZEMBE NA KUBEBA SUPER CUP YA CAF Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top