• HABARI MPYA

  Monday, February 13, 2017

  MWAFRIKA WA KWANZA KULETA MEDALI YA OLIMPIKI AFARIKI DUNIA

  SOKA ya Ghana jana imepata msiba mkubwa kufuatia kifo cha mmoja wa makocha wake mashuhuri, Sam Arday.
  Arday amefariki dunia jana mchana akiwa ana umri wa miaka 71 mjini Accra katika hospitali alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
  Arday aliyekuwa akifahamika kwa jina la utani, “Multi-System Man”, alikuwa kocha wa kwanza kuiongoza timu ya Afrika kutwaa Medali kwenye michuano ya Olympic upande wa soka .
  Ilikuwa ni Medali ya Shaba aliyoipa U-23 ya Ghana katika Olimpiki ya mwaka 1992 mjini Barcelona, Hispania. Timu hya Olimpiki ya Ghana pia ilifika Robo Fainali mwaka 1996 mjini Atlanta, Marekani chini yake.
  Pia aliiwezesha timu ya vijana ya Ghana chini ya umri wa miaka 17 kushinda Medali ya Dhahabu katika Kombe la Dunia la U-17 mwaka 1995 nchini Ecuador. Awali mapema Black Starlets walitwaa ubingwa wa Afrika nchini Mali.
  Pia aliifundisha kwa awamu mbili timu ya taifa ya wakubwa ya Ghana, 1997 hadi 1997 na kwa muda mwaka 2004 katika mechi za kufuzu Kombe la Afrika na Dunia mwaka 2006.
  Arday pia alizifundisha kwa mafanikio klabu mbalimbali za kwao zikiwemo Asante Kotoko, Hearts of Oak, Ashantigold na Okwawu United.
  Hadi anakutwa na umauti alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Chuo cha Soka Afrika Magharibi, zamani kikijulikana kama Fetteh Feyenoord Academy, ambacho kiliibua nyota wengi wa taifa wakiwemo Dominic Adiyiah, Harrison Afful, Jordan Opoku, Nana Akwasi Asare, Philemon McCarthy na wengineo.
  Anakuwa kocha mwingine maarufu wa Ghana kufariki dunia baada ya wengine kama Cecil Jones Attuquayefio, Charles Kumi Gyamfi, Ben Kouffie, Fred Osam Doudu na Emmnauel Afranie.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWAFRIKA WA KWANZA KULETA MEDALI YA OLIMPIKI AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top