• HABARI MPYA

  Tuesday, February 07, 2017

  HANS POPPE AIPONGEZA LIPULI KUREJEA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameipongeza Lipuli ya Iringa kwa kurejea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya miaka mingi.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online jana, Hans Poppe alisema kwamba yeye kama mkazi wa Iringa anajisikia faraja mkoa wake kuwa na timu ya Ligi Kuu tena kwa sasa.
  Alisema kwamba kwa miaka mingi wakazi wa mkoa wa Iringa wamekuwa wakikosa burudani ya Ligi Kuu, lakini hatimaye kuanzia msimu ujao wataanza kuiona ligi hiyo tena.
  Hans Poppe ameipongeza Lipuli ya Iringa kwa kurejea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya miaka mingi

  “Na vizuri zaidi wataishuhudia Ligi Kuu kupitia timu yao kipenzi kabisa, Lipuli. Napenda nichukue fursa kumpongeza kila aliyehusika na kuirejesha timu hii Ligi Kuu. Na ninaomba mshikamano huu uendelee ili kuhakikisha Lipuli inafanya vizuri na kwenye Ligi Kuu pia,”alisema.
  Lipuli imejihakikishia kurejea Ligi Kuu baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Polisi ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kwani imefikisha pointi 46.
  Lipuli inarejea Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu ilipoteremka mwaka 1999, ilipokuwa chini ya kocha Athumani Juma Kalomba, sasa marehemu.       
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HANS POPPE AIPONGEZA LIPULI KUREJEA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top