• HABARI MPYA

  Wednesday, February 01, 2017

  FARID MUSSA AKINUKISHA HISPANIA TENERIFE IKITOA SARE NA ZAMBIA U20

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Farid Malik Mussa jana amecheza dakika zote 90 timu ya vijana ya Tenerife ikilazimishwa sare ya 0-0 na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia katika mchezo wa kirafiki. 
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana kwa simu, Farid alisema kwamba walikutana na timu nzuri ya Zambia katika mchezo mzuri wa kirafiki.
  “Jamaa nilizungimza naop baada ya mechi nikawaambia mimi ninatoka Tanzania, wakafurahi sana na wakaema nitafika mbali nisivunjike moyo, mimi ni mchezaji mzuri,”alisema Farid.
  Farid Mussa jana amecheza dakika zote 90 Tenerife ikilazimishwa sare ya 0-0 na U20 ya Zambia katika mchezo wa kirafiki

  U20 ya Zambia ipo Hispania kwa kambi ya siku 10 kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrikaya Vijana na watacheza pia na U-20 za Las Palmas, Real Madrid na Barcelona.
  Zambia ndiyo wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika la U20 na wataanza kampeni yao ya kuwania taji hilo nyumbani kwa kumenyana na Guinea Februari 26 mwaka 2017 Uwanja wa Heroes.
  Farid alijiunga na klabu hiyo ya Santa Cruz de Tenerife, Tenerife, visiwa vya Canary Desemba mwaka jana kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kutoka Azam FC ya Dar es Salaam. 
  Azam FC ilimtoa kwa mkopo Farid kwenda CD Tenerife kwa makubaliano maalum baada ya winga huyo kufuzu majaribio katika klabu hiyo Aprili mwaka jana alipokwenda na Mkurugenzi wa klabu yake, Yussuf Bakhresa.
  Farid alitua Hispania kwa mara ya kwanza Aprili 21, mwaka jana baada ya kuichezea Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance mjini Tunis, Tunisia ikifungwa 3-0 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam.
  Na ilimchukua wiki moja tu Farid kuwakuna kwa kipaji chake makocha wa Tenerife na kutaka kumnunua, lakini Azam ikakataa na kuamua kumtoa kwa mkopo Desemba, 2016.
  Na baada ya kutua Tenerife amepangiwa kuanza kuchezea kikosi cha U23 ili kupata uzoefu kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza kinachocheza Ligi Daraja la Kwanza nchini humo, maarufu kama Segunda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FARID MUSSA AKINUKISHA HISPANIA TENERIFE IKITOA SARE NA ZAMBIA U20 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top