• HABARI MPYA

  Sunday, February 05, 2017

  EL NENY FITI KUICHEZEA MISRI DHIDI YA CAMEROON

  KOCHA wa Misri, Hector Cuper anaamini kiungo wake nyota, Mohammed El Neny atakuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Cameroon leo.
  Kiungo huyo wa Arsenal hakuwepo wakati Misri inaizifunga Morocco na Burkina Faso katika Robo Fainali na Nusu Fainali kutokana na kuwa majeruhi.
  "Nina furaha El Neny yupo kwwa ajili ya fainali baada ya timu ya madaktari kumthibitisha yuko vizuri kiafya. Kukosekana kwake lilikuwa pengo kubwa na vizuri kuwa naye tena baada ya maumivu yake,"alisema Hector Cuper.
  Kwa upande wake, El Neny alikuwa mwenye furaha kurejea na kusema, "Ni nafuu kubwa na ninamshukuru Allah (Mungu). Umekuwa wakati mgumu kukosa mechi muhimu za nchi yangu, lakinin hatimaye sasa nipo,".
  Pamoja na hayo, daktari wa timu, Ayman Aboul-Ela amesema beki wa kushoto Mohamed Abdel-Shafi, ambayeb aloiumi kifundo cha mguu Misri ikiifunga 1-0 Uganda kwenye mchezo wa kundi lao, hatakuwapo kwenye fainali leo=.
  Wakati huo huo: Bao pekee la Alain Traore dakika ya 88 jana lilitosha kuipa Burkina Faso nafasi ya tatu AFCON 2017 baada ya kuilaza Ghana 1-0 Uwanja wa Port-Gentil.
  Vikosi vilikuwa; Ghana: R. Ofori, Yiadom, Menash, Partey, Badu, J. Ayew/Atsu dk74, Tekpetey/A. Ayew dk69, E. Ofori, Amartey, Tetteh/Gyan dk64 na Afful
  Burkina Faso: Koffi, Yago, B. Kone, Nakoulma, S. Traore. Dayo, Bance/Cyrille dk73, Kabore, B. Traore, Yacouba/Malo dk83 na I. Traore.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EL NENY FITI KUICHEZEA MISRI DHIDI YA CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top