• HABARI MPYA

  Tuesday, February 07, 2017

  CHECHE APIGA HESABU ZA KUZIPOROMOSHA SIMBA, YANGA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Iddi Nassor Cheche amesema kwamba ushindi wa jana wa 1-0 dhidi ya Ndanda FC umekuwa mwendelezo mzuri wa wimbi lao la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na sasa wanazikazia mwendo Yanga na Simba kileleni.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online juzi, Cheche alisema kwamba ushindi huo unaofuatia ushindi wa 1-0 pia dhidi ya Simba ni chachu kwao kushinda mechi zijazo pia.
  “Nimeupokea kwa furaha ushindi huu, nawapongeza sana wachezaji wangu kwa kazi nzuri waliofanya leo, hususan mfungaji wa bao (Yahya Mohammed),”alisema.
  Pamoja na hayo, Cheche amewataka wachezaji wake kukaza msuli kuelekea mechi zijazo, kwani wanazidiwa kwa pointi nyingi na wapinzani Azam na Yanga.
  “Bado tuna kazi kubwa, tuna kazi kubwa sababu tunazidiwa pointi nyingi na timu zilizo mbele yetu, Yanga na Simba, kwa hiyo tunatakiwa kuendeleza wimbi la ushindi ili tuwafikie kama na wao watateleza huko mbele ya safari,”alisema. 
  Baada ya kuipiga Ndanda bao 1-0 juzi usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Azam FC inafikisha pointi 37 baada ya kucheza mechi 21 na inaendelea kushika nafasi ya tatu.
  Iko nyuma ya Yanga ambayo inayongoza kwa pointi zake 49, ikifuatiwa na Simba yenye pointi 48 baada ya timu zote kucheza mechi 21 pia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHECHE APIGA HESABU ZA KUZIPOROMOSHA SIMBA, YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top